Tasnifu hii inahusu dhana ya uchimuzi katika uendelezaji wa riwaya ya kimajaribio au mpya ya Mafamba (2008). i riwaya ya kwanza ya Olali inayomulika hali ya kisiasa katika jamii yetu na harakati za wananchi za kuwangoa viongozi wadhalimu. Katika kuitafiti kazi hii, tuliongozwa na mwelekeo wa kihakiki wa Urasimu wa Kirusi. Utafiti huu unahusu nafasi ya uchimuzi katika nwaya ya Mafamba. Suala ambalo tumeshughulikia kwa kuangazia uchimuzi katika ngazi ya wahusika na rnatumizi ya lugha. Utafiti huu ulilenga kudhihirisha kuwa, uchirnuzi ni nguzo kuu katika uendelezaji wa riwaya ya kimajaribio au mpya ya Mafamba. Tumeigawa tasnifu hii katika sura tano. Iii kufikia malengo yetu. sura ya kwanza imeshughulikia utangulizi kwa ujumla. Utangulizi huu unahusu usuli wa mada. tatizo la utafiti. madhumuni ya utafiti, nadharia tete, sababu za kuchagua mada, mipaka na upeo, misingi ya kinadharia, yaliyoandikwa kuhusu mada yetu na njia za utafiti. Katika sura ya pili. tumezungumzia msuko wa riwaya ya Mafamba ambao unajenga msingi wa uelewa wa riwaya hii. Tumeiona riwaya hii kuwa ya kuvutia na' kusisirnua hasa kutckana na usimulizi wake unaoelezea masuala nyeti ya kisiasa ya jamii yetu katika mtindo mpya wa uandishi kwa njia inayokiuka sifa za uandishi wa riwaya za jadi. Katika sura ya tatu tumeshughulikia uchimuzi katika k iwango cha wahusika. chimuzi huu unatokea katika kiwango cha maana au kisemantiki. Tumebainisha kwamba, uchimuzi wa wahusika katika riwaya ya Mafamba unabainika kupitia kwa usawiri wao kiasi cha kubatilisha clhana nzima ya uhusika hata ingawa matendo yao na wasifu wao unachukuana na hali ya kisasa ya maisha ya jamii yetu kwa jinsi tunapata kuwatambua, kutambua tabia zao na rnielekeo yao. Aidha kupitia kwa uchirnuzi katika kiwango hiki. dharnira ya mwandishi na aidha maudhui katika riwaya hii yanabainika. Sura ya tatu inahusu uchimuzi katika kiwango cha matumizi ya lugha. Ili kufanikisha lengo letu, tuliangazia vipengele vya matumizi ya lugha katika kiwango cha kimsamiati na kisernantiki. Utafiti wetu umebaini kuwa, viwango hivi vinachimuza sifa zilizozungumziwa na Wana- Urasimu kama uajinabishaji au kufanya kazi ya kifasihi kuonekana kuwa ngeni, matumizi ya mbinu kadha za uwasilishaji na rnatumizi ya kipekee ya lugha. , Sura ya tano inahusu hitimisho la utafiti. Katika sehemu hii, tumerejelea mada ya utafiti huu na maswala ya kimsingi tuliyoyaelezea katika sura ya kwanza. Kutokana na matokeo ya uchanganuzi data yetu, tumerejelea nadharia tete zetu ili kuzikubali na pia tumetoa mahitimisho na mapendekezo ya utafiti wa baadaye.
Level: post-graduate
Type: dissertations
Year: 2012
Institution: University of Nairobi
Contributed by: zemuhindi
Join Whatsapp channel
info@asbatdigitallibrary.org
Plot 3, KTS Road Makerere University after Infectious Diseases Institute