Utafiti huu ulichunguza muundo wa simulizi kwenye riwaya ya Vuta N’kuvute yake Adam Shafi. Utafiti wetu ulikuwa na malengo ambayo ni kuchunguza muundo wa simulizi katika riwaya ya Vuta N’kuvute, kuonyesha jinsi vipengele vya hadithi, matini na usimulizi vinavyodhihirika katika riwaya hiyo na kubainisha uamilifu wa vipengele vya simulizi katika kujenga ukamilifu wa riwaya ya Vuta N’kuvute. Utafiti uliongozwa na nadharia ya Naratolojia mtazamo wa Rimmon-Kenan (2002). Mihimili ya nadharia hii ndiyo iliongoza kwenye utafiti kwani ilisaidia kwenye uchunguzi wa usawiri wa wahusika na uwasilishaji wa usemi na mawazo yao. Vilevile, ilisaidia kuelewa jinsi kipengele cha wakati kinavyojitokeza kwenye riwaya ya Vuta N’kuvute na kubaini jinsi usimulizi na mtazamo unavyojitokeza. Utafiti ulikuwa wa maktabani na uchanganuzi na uwasilishwaji wa data ulikuwa kwa mbinu ya maelezo. Mapendekezo yaliyotolewa kwenye utafiti wetu ni kuwa, tafiti za baadaye zifanywe kuhusu riwaya zingine za Adam Shafi na pia tafiti za kiulinganishi kama vile kwenye riwaya na hadithi fupi kuhusu muundo wa simulizi.
Level: post-graduate
Type: dissertations
Year: 2022
Institution: University of Nairobi
Contributed by: zemuhindi
Join Whatsapp channel
info@asbatdigitallibrary.org
Plot 3, KTS Road Makerere University after Infectious Diseases Institute