Show abstract

MATUMIZI YA USHAIRI KATIKA TAMTHILIYA ZA KISWAHILI: KIMYA KIMYA, KILIO CHA HAKI NA MKE MWENZA

Utafiti huu ulikusudia matumizi ya ushairi katika tamthiliya za Kiswahili. Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa ni kuonyesha jinsi ushairi unavyo tumiwa katika tamthiliya za kiswahili, na madhumuni mahususi yaani kuonyesha athari zilizopo katika utumishi wa ushairi katika tamthilya, kuchunguza dhima na sababu za kutumia ushairi katika tamthiliya za kiswahili na kuonyesha changamoto zinazokumba utumiaje wa ushairi katika tamthiliya za kiswahili. Utafiti huu pia ulikuwa na maswali kama, ni nini chimbuko lakutumia mashairi katika tamthilia za Kiswahili?, Je, mashairi yameathiri wasomaji wa tamthilia za kiswahili?. Utafiti huu ulifanyiwa katika nchini Uganda hasa katika vitabu vya tamthilia za kiswahili vilivyomo makitabani ya Chuo kikuu Cha Makerere. Utafiti huu ulikuwa na umuhimu wa kusaidia jamii kwa kutambua matumizi ya ushairi katika tamthilia za Kiswahili afrika mashariki, kusaidia mtafiti kukusanya data na kuihifadhi katika maandishi, matokeo ya utafiti huu yatasaidia watafiti wengine kama marejeleo na matokeo ya utafiti huu yalisaidia idara ya lugha na mawasiliano kutambua kuwa mtafiti alienda maktabani. Mbinu mbili za ukusanyaji data zilitumiwa ambazo ni; maktabani na uchunguzi shirikishi. Utafiti huu ulingunduwa kwamba mashairi ya mitumiwa katika tamthilia za Kiswahili katika maendeleo ya fasihi. Utafiti huu ulitoa hitimisho kwamba Ushairi unatumiwa katika tamthiliya za Kiswahili katika Afrika Mashariki na sehemu zingine za dunia inaendelea baada ya kuchunguza hatua ambazo zinaendeleza ushairi wa Kiswahili.

more details

Author: bwambale biino
Contributed by: asbat digital library
Institution: makerere university
Level: university
Sublevel: under-graduate
Type: dissertations