Show abstract
LUGHA KATIKA KATIBA YA KENYA: UJITOKEZAJI WAKE KATIKA UTANGAZAJI WA JANGA LA UVIKO-19
Safari ya kukamilisha utafiti huu ilikuwa na changamoto si haba, ila nashukuru kwa ushauri, maelekezo na mawazo ya watu mbalimbali. Mchango wao mkubwa ulipunguza changamoto ambazo zilihusiana na utafiti huu. Natoa shukrani zangu kwa Mungu kwa neema yake katika kipindi hiki cha shahada ya uzamili na kuniwezesha kuikamilisha. Kwa neema ya Mungu tuliweza kuikamilisha tasnifu hii. Ningependa kuwashukuru wasimamizi wangu, Dkt. Mukhwana na Prof. Iribe Mwangi kwa kujitolea kwao kusoma na kunipa marekebisho yaliyonifaa si haba katika kukamilisha kazi hii. Walijitolea kwa hali na mali kunielekeza ipasavyo. Walinihudumia kila nilipowahitaji ingawa walikuwa na majukumu si haba chuoni na katika familia zao. Nawashukuru kwa mawaidha na maelekezo yao ya kitaaluma ambayo yalinifaa. Mungu awabariki na awaongezee hekima. Nawashukuru watoto wangu, Javan Miruka, Nethanel Nyangoto na Shanezah Sarange kwa kunivumilia kipindi cha utafiti wangu. Nililazimika kushughulikia utafiti wangu na kuwanyima nafasi ya kutangamana nao hata wakati wa usiku. Nawashukuru ndugu zangu kwa kusimama nami katika kipindi cha utafiti huu. Vile, siwezi kuwasahau rafiki zangu kama vile Ruth Binyanya na Dorca Getonto kwa kunipa moyo hata wakati nilikuwa nimekosa tumaini la kukamilisha tasnifu yangu. Mungu awabariki. Siwezi kuwasahau pia Hellen Bitutu, Ben Nyang’ate, Vanesa Nyang’arisa, Diana Bosibori , Nixon Ntabo na Yvonne sarange kwa msaada wao. Nawatakia maisha mema.
more details
- download pdf
- 0 of 0
- 150%