Show abstract

TAMAA NA ATHARI ZAKE KATIKA JAMII: ULINGANISHI WA UA LA FARAJA NA PARADISO

Katika tasnifu hii, tumeshughulikia tamaa na athari zake katika jamii: ulinganishi wa Ua la Faraja ya W. E. Mkufya (2008) na Paradiso ya J. Habwe (2014). Tumetumia nadharia ya maadili kuhakiki kazi hizi. Tasnifu hii yetu ina sura tano. Katika sura ya kwanza, tumeeleza sehemu kama usuli wa utafiti, sababu za kushughulikia mada hii, upeo na mipaka ya utafiti, maswali ya utafitii, malengo ya utafiti, tatizo la utafiti, yaliyoandikwa kuhusu mada, nadharia ya maadili iliyotumiwa kuhakiki kazi hizi na mbinu za utafiti. Katika sura ya pili, tumeshughulikia lengo la kwanza, namna dhamira ya tamaa imekuzwa na kuendelezwa katika riwaya hizi Katika sura ya tatu tumebainisha athari zinazotokana na tamaa na ambazo zinaikumba jamii katika kazi hizi mbili. Vilevile, katika sura ya nne, tumebainisha ushauri uliopendekezwa katika riwaya zote mbili ili kukabiliana na tamaa na athari zake katika jamii. Sura ya tano inaeleza kuhusu matokeo ya utafiti pamoja na mapendekezo kuhusu utafiti huu. Mwisho kuna marejeleo ya utafiti huu

more details

Author: akong’o, thomas o
Contributed by: zemuhindi
Institution: university of nairobi
Level: university
Sublevel: post-graduate
Type: dissertations